Zaidi
ya ekari 2 za miti zimetolewa na kijiji
cha Isapulano wilayani Makete mkoani
Njombe kwa mwenyekiti mstaafu na mwanzilishi
wa kijiji hicho Mzee Kasambala Mwakilama
Sanga
Wakikabidhi
msitu wenye thamani ya zaidi ya tsh, milioni 3 wajumbe wa kamati ya kijiji cha
Isapulano wamesema wametoa zawadi hiyo kwa Mzee Kasambala kama kumbukumbu ya
kuenzi uongozi wake tangu mwaka 1968 hadi kufikia mwaka 1992 hadi kustafu mwaka
ambapo alistaafu rasmi
Kwa
upande wao baadhi ya wananchi wa kijiji hicho wamempongeza Mzee Kasambala kwa kazi
kubwa alizofanya ikiwa ni pamoja na
kujenga shule ya msingi Isapulano.
Akizungumza kwa niaba ya familia ya Mzee Kasambala mwalimu
Tobiasi Sanga amekiri kupokea zawadi hiyo na kuwataka viongozi wengine
kuendelea kuenzi wazee ili kuwafanya wasivunjike moyo katika maisha yao ya
uzee.
Aidha
akizungumza kwa niaba ya wananchi wa Isapulano mwenyekiti wa kijiji Bw,Imani Nasekile
Tweve amesema ofisi ya kijiji wataendelea kuenzi na kukumbuka umuhimu wa kazi
zilizo fanywa na wazee katika kuleta maendeleo ya kijiji akiwemo mzee Kasambala.
Katika
hatua nyingine mh. diwani wa kata ya Isapulano Bw. Aginiwe Mahenge ametoa wito kwa wananchi wa wilaya ya Makete
kuwaenzi wazee kwa kuwapa motisha wa zawadi yeyote ile kutokana na kazi
walizozifanya kwa kijiji na taifa kwa ujumla
Na
Aldo Sanga.
Post a Comment