CCM MAKETE YAUNGA MKONO KAULI YA NAPE NNAUYE KUHUSU VIONGOZI WASIOWAJIBIKA

Wednesday, November 20, 20130 comments

Kufuatia kauli iliyotolewa na katibu mwenezi na itikadi wa CCM Taifa Ndugu Nape Nnauye kuhusina na baadhi ya Mawaziri kutoka chama  cha mapinduzi CCM kutowajibika kwenye nyadhifa zao na kushindwa kutatua kero za wananchi hatimaye katibu wa Chama cha Mapinduzi wilaya ya Makete Bw.Miraji Mtaturu (Pichani) ameunga mkono kauli hiyo na kusema suala la uwajibikaji lazima lifuatiliwe ili kuwafikishia huduma bora wananchi.
 
Akizungumza na blog hii mapema hii leo Bw.Mtaturu amesema anaunga mkono kauli hiyo na kumpongeza kiongozi huyo kwa uamuzi aliouchukua na kuhusisha uwajibikaji kwa baadhi ya viongozi wa wilaya ya Makete ambao hawawajibiki ipasavyo katika utekelezaji wa shughuli za maendeleo hususani katika mradi wa maji uliofadhiliwa na Benki ya Dunia uliopo katika tarafa ya Matamba.
Na Fadhili Lunati 
Share this article :

Post a Comment

 

Copyright © 2013. MAKETE BLOG - All Rights Reserved
Designed by Edwin Moshi
Property of Makete District Council