Kikundi cha ngoma cha WANGAMA kikitumbuiza kwenye uzinduzi huo.
Katibu tawala mkoa wa Njombe Mgeni Baruani (kulia) akipata maelezo kwenye kituo cha afya Makambako baada ya uzinduzi huo
Jamii
imeshauriwa kuwahimiza akina mama wajawazito kuenda kwenye vituo vya
huduma za afya mapema ili kuchunguzwa afya zao na endapo watabainika
kuwa na maambukizi ya virusi vya UKIMWI wataanzishiwa dawa za kuzuia
maambukizi ya virusi hivyo kutoka kwa mama kwenda kwa mtoto
Rai
hiyo imetolewa na katibu tawala mkoa wa Njombe Bi. Mgeni Baruani kwenye
uzinduzi wa kampeni ya tokomeza maambukizi ya virusi vya UKIMWI kutoka
kwa mama kwenda kwa mtoto uzinduzi katika kituo cha afya Makambako
mkoani Njombe
Bi.
Baruani amesema dawa hizo za kuzuia maambukizi ya virusi vya Ukimwi
toka kwa mama kwenda kwa mtoto zinatolewa bure kwenye vituo vya kutolea
huduma za afya mkoani Njombe na Iringa hivyo kuitaka jamii kushirikaina
na serikali kuokoa maisha ya kina mama wajawazito na watoto wao
watarajiwa
Pia
amehimiza viongozi wote na vyombo vya habari kuongeza nguvu ya
kuwahimiza wananchi wajitokeze kupima afya zao kwani bado anaamini kwa
dhati kuwa Tanzania bila UKIMWI inawezekana
"Wito
wangu kwa wenzi shirikianeni kuwakinga dhidi ya maambukizi watoto
wenu.kwa kiongozi nawaombeni wote kuanzia ngazi ya kaya hadi mkoa muwe
mstari wa mbele katika mapambano dhidi ya vvu hususan kutoka kwa mama
kwenda kwa mtoto, kwani pia ni jukumu la kila mmoja wetu kwenye jamii
kuhakikisha kuwa tunawanusuru watoto na maambukizi haya" alisema Mgeni
Awali
akisoma taarifa ya uzinduzi huo mratibu wa UKIMWI halmashauri ya mji wa
Makambako Bi. Magdaleth Msasi amesema mpango huo utafuatwa vizuri ni
dhahiri kuwa kuna mafanikio katika kupunguza maambukizi ya vvu toka kwa
mama kwenda kwa mtoto katika mkoa wa Njombe na Iringa
Aidha
alisema ni vyema kina mama wajawazito kuendelea kujifungulia kwenye
vituo vya kutolea huduma ya afya ya uzazi na mtoto chini ya usimamizi wa
mhudumu wa afya kwani itamhakikishia kujifungua kwa usalama vilevile
kupewa elimu ya namna ya kuzuia maambukizi kwa mtoto anayetarajiwa
kuzaliwa na ambaye amezaliwa tayari
Mpango
huo uliozinduliwa kwa mikoa ya Njombe na Iringa unalenga kupunguza
maambukizi mapya ya VVU kwa asilimia 50 miongoni mwa wanawake wenye umri
wa kuzaa (15-49) na pia kuongeza na kuboresha upatikanaji wa huduma za
uzazi wa mpango miongoni mwa akina mama wanaoishi na VVU.
Habari/picha na Veronica Mtauka,www.edwinmoshi.com, Makambako.
Post a Comment