Moja ya alama zilizowekwa na idara ya ardhi kwenye eneo walilopimiwa wafanyabiashara hao.
Eneo lililotengwa na halmashauri kwa ajili ya kujenga mabanda ya biashara.Picha na Edwin Moshi
=====
Zoezi la Upimaji na Ugawaji
wa Viwanja eneo la Soko Kuu Makete mjini kwa wafanyabiashara waliobomolewa Vibanda
wilayani Makete Mkoani Njombe
limekamilika rasmi kwa Wafanyabiashara hao na Kukabidhiwa
Viwanja hivyo kwa ajili ya kuanza Rasmi Ujenzi Huo.
Hayo yamesemwa na Afisa Ardhi
wilaya ya Makete Bw. Anikas Vilumba wakati alipokuwa akifanya Shughuli ya
Upimaji wa Viwanja Hivyo kwa Wafanyabiashara hao
Amesema kuwa Endapo
wafanyabiashara watajitokeza katika eneo hilo la Viwanja watakabidhiwa viwanja vyao kwa ajili
ya kuanza Rasmi kwa Ujenzi wa Vibanda vya Biashara kwa walioathirika na zoezi
na bomoabomoa kupisha ujenzi wa barabara kwa kiwango cha lami.
Habari na Fadhili Lunat
Post a Comment