Afisa elimu sekondari
wilayani Makete mkoani Njombe Bwana Jacob Meena
amesema kuwa hali ya mitihani ya kidato cha nne inayoendelea kwa
sasa wilayani Makete na Tanzania nzima,
kwa upande wa wilaya ya Makete hali ya ufanyaji wa mitihani hiyo haina dosari
yoyote hadi hivi sasa
Akizungumza na kitulo fm inayomilikiwa na halmashauri ya Makete ofisini
kwake Bwana Meena amesema kuwa hakuna tatizo lolote lile lililoripotiwa ofisini
kwake kuhusu mitihani inayoendelea
Hata hivyo amesema kuwa kuna
aina tatu za watahiniwa waliosajiliwa kufanya mitihani hiyo ikiwa ni watahiniwa
wa shule(wanafunzi waliokuwepo shuleni kwa kipindi cha miaka minne ),watahiniwa
wa kujitegemea na mtihani wa maarifa
Akitoa idadi ya watahiniwa
ambao wamesajiliwa kufanya mitihani hiyo wilayani hapa amesema jumla ya
wanafunzi ni 1,245 ambapo wanafunzi wa shule ni 1,094 na watahiniwa wa kujitegemea
pamoja na maarifa ni 151
Hata hivyo Bw.Meena ametoa
wito kwa wanafunzi hao kuwa watumie akili yake ktk ufanyaji wa mitihani hiyo na
siyo kutazamia kwa mwenzake kwani akikamatwa hatua za kisheria zitachukuliwa
dhidi yake
Na Benson Kyando
Post a Comment