MBUNGE WA MAKETE DKT. BINILITH MAHENGE ATEKELEZA AHADI YAKE ALIYOITOA KATIKA KATA YA ISAPULANO

Wednesday, November 20, 20130 comments

Umoja wa wanawake wa chama cha mapinduzi kata ya Isapulano wamekabidhiwa mradi wa nguruwe wenye thamani ya shilingi laki mbili na themanini  na Mh.diwani wa kata ya Isapulano Aginiwe Mahenge kwa niaba ya Mbunge wa Jimbo la Makete
Akikabidhi nguruwe hao kwa niaba ya mbunge Binilith Mahenge ambaye ni mbunge wa jimbo la Makete, diwani huyo amewataka wana kikundi hicho kutunza nguruwe hao ili kuendelea kuongeza kipato ili waweze kujikwamua kwenye wimbi la umasikini.
Kwa upande wake mwakilishi wa kikundi hicho Bi. Etelinah Mahenge amemshukuru Mh. mbunge kwa kutoa msaada huo na kuahidi kuwa watautunza mradi huo kwa hali na mali ili kuongeza kipato katika maisha yao.
Nguruwe hao wametolewa na mh. mbunge wa Makete ikiwa ni ahadi yake aliyoitoa tarehe kumi na tano septemba mwaka huu wakati wa ziara yake kijiji hapo. 
Na Riziki Manfred
Share this article :

Post a Comment

 

Copyright © 2013. MAKETE BLOG - All Rights Reserved
Designed by Edwin Moshi
Property of Makete District Council