PICHA:KINANA NA UJUMBE WAKE WATEMBELEA UJENZI WA SHULE MPYA YA SEKONDARI YA WASICHANA UKWAMA, MAKETE

Saturday, December 07, 20130 comments

Katibu mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana(kulia) akisalimiana na Bw. Titho Tweve ambaye analeta saruji ya kuendelea na ujenzi wa majengo ya shule ya sekondari ya wasichana Ukwama, wa kwanza kushoto ni katibu NEC itikadi na uenezi Nape Nnauye akifuatiwa na katibu wa NEC siasa na mahusiano ya kimataifa Dkt. Asharose Migiro
Mkuu wa wilaya ya Makete Mh. Josephine Matiro (katikati) akitoa maelezo kwa katibu mkuu wa CCM kuhusu ujenzi wa shule hiyo
 Katibu mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana akizungumza mara baada ya kupata taarifa ya ujenzi huo, ambapo ameahidi kuwa chama cha mapinduzi kitatoa mabati 200 kwa ajili ya shule hiyo
Moja ya darasa la shule hiyo likiwa limekamilika kwa ujenzi
Msafara wa katibu mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana ukiondoka kwenye shule ya sekondari ya wasichana Ukwama, tayari kuelekea wilaya ya Wanging'ombe kwa ajili ya shughuli nyingine za kichama.Picha zote na Edwin Moshi
Share this article :

Post a Comment

 

Copyright © 2013. MAKETE BLOG - All Rights Reserved
Designed by Edwin Moshi
Property of Makete District Council