Mkuu wa wilaya ya Makete Josephine Matiro akikagua gwaride la wanamgambo
Mkuu wa wilaya akitoa hotuba yake
Vijana wilayani Makete mkoani Njombe
wametakiwa kutambua kuwa suala la wao kushiriki mafunzo ya mgambo lipo
kisheria hivyo kuitaka jamii kwa ujumla kushirikiana ili malengo ya
mafunzo hayo yatimie
Rai hiyo imetolewa na mkuu wa wilaya ya
Makete Bi Josephine Matiro wakati akifunga mafunzo ya mgambo
yaliyofanyika kwa kipindi cha miezi minne katika kata ya Lupila wilayani
Makete
Bi Matiro amefikia hatua hiyo kutokana
na risala ya mgambo hao kuonesha kuwa wapo walioandikishwa kushiriki
mafunzo hayo lakini waliyakatisha kutokana na sababu mbalimbali ikiwemo
uvivu na kutoona umuhimu wa mafunzo hayo ambapo awali waliandikishwa
zaidi ya 150 lakini wamehitimu 61 tu
Katika hatua nyingine Mkuu wa wilaya
amewashauri mgambo hao kuanzisha kikundi chao cha ujasiriamali na endapo
watafanya hivyo serikali itawapatia mikopo itakayowasaidia kujiendessha
kupitia vikundi
Wakizungumza
na mtandao huu baadhi ya mgambo waliohitimu kwenye mafunzo wameshukuru
na kusema kuwa wameelewa mambo mengi ikiwemo kutumia silaha, kukabiliana
na adui hata kama ana silaha, mbinu za kivita pamoja na huduma ya
kwanza
Na Edwin Moshi
Post a Comment