skip to main |
skip to sidebar
WAFANYABIASHARA WALIOBOMOLEWA VIBANDA VYAO MAKETE MJINI WAZIDI KUOMBA VIWANJA
Kutokana
na zoezi la bomoa bomoa lililofanyika Makete mjini Wafanyabiashara wamejitokeza kujaza fomu za kuomba viwanja
vilivyotangazwa Oktoba 17 mwaka huu na mkurugenzi mtendaji wa
halmashuri ya wilaya ya Makete Bwana Iddi Nganya hadi sasa ni watu 28 tu
waliomba fomu kwa kibali kutoka katika ofisi ya kata ya Iwawa.
Mwenyekiti wa wafanyabiashara wilayani Makete Bwana Hosea Mpandila amesema
kuwa wafanyabiashara walio bomolewa vibanda ni 42 na waliojitokeza
kujenga vibanda vipya ni 35 na wafanyabiashara 7 hawajulikani
walipokwenda
Pia ameongeza kuwa sehemu ambazo wamesambaza fomu
hizo ni pamoja na Kona fomu 6 Mabehewani fomu 58 soko kuu la Makete
mjini fomu 60 na Dombwela hawajafuatilia fomu hizo hadi sasa ilikuweza
kuzichukua kwa mwenyekiti huyo
Picha na Edwin Moshi, habari kwa hisani ya Kitulo FM
Post a Comment