Wazazi
na walezi wilayani makete Mkoani Njombe wametakiwa kusimamia maadili ya
vijana wao na kuhakikisha wanakwenda katika mstaari ulionyooka ili
kuondokana na matatizo yanayowapata ambayo pengine yangeweza kuepukika
Hayo
yamesemwa na naibu katibu mkuu wa umoja wa wanawake Tanzania (UWT) Eva
Kihwele katika mkutano wa hadhara alioufanya katika kata ya Luwumbu
wilayani hapa baada ya kutembelea miradi mbalimbali ya maendeleo katika
kata hiyo
Bi
Kihwele amesema inashangaza kuona wazazi hasa kina baba wamekuwa mstari
wa mbele kuwapiga wake zao kwa madai kuwa wamewakosea lakini
wanashindwa kuwaadhibu watoto wao wanaovaa nguo zisizo na maadili ya
kitanzania
"Unakuta
mtoto wa kike kavaa kimini ama nguo za kubana mpana wewe kama mzazi
unaona aibu kumtazama, wa kiume kavaa mlegezo, lakini hamuwakemei na
badala yake mnawapiga wake zenu tu kwanini? alisema Kihwele
Amewataka
wazazi kuwa mstari wa mbele kuwajenga watoto wao kitabia ili wavae
mavazi yenye maadili ya kitanzania ili pamoja na mambo mengine iwe
rahisi kwao hata kupata ajira mara baada ya kumaliza masomo yao
Katika
hatua nyingine amewataka wazazi kuacha tabia ya kuwaruhusu watoto wao
kwenda Dar es Salaam kufanya kazi za ndani kwa madai kuwa ni kuzuri, na
badala yake watoto hao huenda kuishi maisha magumu huko na mwishowe
wanajiingiza katika vitendo vya kuuza miili yao hivyo kuwaweka katika
hatari ya kupata maambukizi ya virusi vya UKIMWI
Naibu katibu UWT Taifa yupo wilayani Makete kuendelea na ziara yake ambapo hii leo ametembelea
kata za Luwumbu na Ipelele na kutembelea mashamba darasa, mfereji wa
umwagiliaji pamoja na ujenzi wa bweni la wanafunzi Ipelele sekondari na
kufanya mikutano ya hadhara katika kata hizo
Na Edwin Moshi
Post a Comment