MWENYEKITI MSTAAFU WA KIJIJI CHA ISAPULANO MAKETE APEWA ZAWADI YA MSITU WA MAMILIONI YA FEDHA

Thursday, November 07, 20130 comments

Zaidi ya ekari 2 za miti  zimetolewa na kijiji cha Isapulano  wilayani Makete mkoani Njombe kwa mwenyekiti mstaafu  na mwanzilishi wa kijiji hicho  Mzee Kasambala Mwakilama Sanga

Wakikabidhi msitu wenye thamani ya zaidi ya tsh, milioni 3 wajumbe wa kamati ya kijiji cha Isapulano wamesema wametoa zawadi hiyo kwa Mzee Kasambala kama kumbukumbu ya kuenzi uongozi wake tangu mwaka 1968 hadi kufikia mwaka 1992 hadi kustafu mwaka ambapo alistaafu rasmi

Kwa upande wao baadhi ya wananchi wa kijiji hicho wamempongeza Mzee Kasambala kwa kazi kubwa alizofanya  ikiwa ni pamoja na kujenga shule  ya msingi Isapulano.

Akizungumza  kwa niaba ya familia ya Mzee Kasambala mwalimu Tobiasi Sanga amekiri kupokea zawadi hiyo na kuwataka viongozi wengine kuendelea kuenzi wazee ili kuwafanya wasivunjike moyo katika maisha yao ya uzee.


Aidha akizungumza kwa niaba ya wananchi wa Isapulano mwenyekiti wa kijiji Bw,Imani Nasekile Tweve amesema ofisi ya kijiji wataendelea kuenzi na kukumbuka umuhimu wa kazi zilizo fanywa  na wazee katika kuleta  maendeleo ya kijiji akiwemo mzee Kasambala.

Katika hatua nyingine mh. diwani wa kata ya Isapulano Bw. Aginiwe  Mahenge ametoa wito kwa wananchi wa wilaya ya Makete kuwaenzi wazee kwa kuwapa motisha wa zawadi yeyote ile kutokana na kazi walizozifanya kwa kijiji na taifa kwa ujumla

Na Aldo Sanga.
Share this article :

Post a Comment

 

Copyright © 2013. MAKETE BLOG - All Rights Reserved
Designed by Edwin Moshi
Property of Makete District Council