ZOEZI LA KUGAWA VIWANJA KWA WAFANYABIASHARA WALIOBOMOLEWA VIBANDA VYAO MAKETE MJINI LAKAMILIKA

Saturday, November 16, 20130 comments

Moja ya alama zilizowekwa na idara ya ardhi kwenye eneo walilopimiwa wafanyabiashara hao.
 Eneo lililotengwa na halmashauri kwa ajili ya kujenga mabanda ya biashara.Picha na Edwin Moshi
=====
Zoezi la Upimaji na Ugawaji wa Viwanja eneo la Soko Kuu Makete mjini kwa wafanyabiashara waliobomolewa Vibanda wilayani  Makete Mkoani Njombe limekamilika rasmi kwa Wafanyabiashara hao na Kukabidhiwa Viwanja hivyo kwa ajili ya kuanza Rasmi Ujenzi Huo.
Hayo yamesemwa na Afisa Ardhi wilaya ya Makete Bw. Anikas Vilumba wakati alipokuwa akifanya Shughuli ya Upimaji wa Viwanja Hivyo kwa Wafanyabiashara hao
Amesema kuwa Endapo wafanyabiashara watajitokeza katika eneo hilo la Viwanja watakabidhiwa viwanja vyao kwa ajili ya kuanza Rasmi kwa Ujenzi wa Vibanda vya Biashara kwa walioathirika na zoezi na bomoabomoa kupisha ujenzi wa barabara kwa kiwango cha lami.
Habari na Fadhili Lunat
Share this article :

Post a Comment

 

Copyright © 2013. MAKETE BLOG - All Rights Reserved
Designed by Edwin Moshi
Property of Makete District Council