Kufuatia kauli iliyotolewa na
katibu mwenezi na itikadi wa CCM Taifa Ndugu Nape Nnauye kuhusina na baadhi ya Mawaziri
kutoka chama cha mapinduzi CCM
kutowajibika kwenye nyadhifa zao na kushindwa kutatua kero za wananchi hatimaye
katibu wa Chama cha Mapinduzi wilaya ya Makete Bw.Miraji Mtaturu (Pichani) ameunga mkono
kauli hiyo na kusema suala la uwajibikaji lazima lifuatiliwe ili kuwafikishia
huduma bora wananchi.
Akizungumza na blog hii mapema hii leo Bw.Mtaturu amesema anaunga mkono kauli hiyo na kumpongeza kiongozi huyo kwa uamuzi aliouchukua na kuhusisha uwajibikaji kwa baadhi ya viongozi wa wilaya ya Makete ambao hawawajibiki ipasavyo katika utekelezaji wa shughuli za maendeleo hususani katika mradi wa maji uliofadhiliwa na Benki ya Dunia uliopo katika tarafa ya Matamba.
Na Fadhili Lunati
Post a Comment