Mtu mmoja mkazi wa kijiji cha
Ilevelo kata ya Lupalilo Bw.Alfred Sanga amejeruhiwa na mnyama anayesadakiwa kuwa ni nyati hii leo
majira ya saa 3 asubuhi kijijini hapo
Akihibitisha kutokea kwa tukio
hilo M/kiti wa kijiji hicho Bw.Festo Mahenge
amesema kuwa tukio hilo
limetokea mnamo saa 3 asubuhi wakati Bw.Alfred sanga akiwa anaelekea machungoni
kwa ajili ya kuangalia Ng’ombe wake ndipo alipomkuta mnyama huyo aina ya nyati
akiwa amelala na ghafla alizinduka na kumjeruhi eneo la shingo yake
Amesema majeruhi huyo alipata
nafasi ya kukimbia na ndipo akapelekwa Hospitali ya Mission ya Ikonda iliyopo kata ya Tandala wilayani Makete kwa
matibabu zaidi,imeelezwa kuwa amehudumiwa na kuruhusiwa kurudi nyumbani kwake
ambapo hali yake hadi hivi sasa inaendelea vizuri
Hata hivyo M/kiti wa kijiji
hicho Bw.Mahenge amesema kuwa ni hali ya kushangaza kutokea kwa mnyama
huyo kijijini hapo kwani ni mara ya kwanza ambapo amesema kuwa mnyama
huyo inasadikika ametokea mpakani mwa kijiji jirani cha Mago na Ugabwa
Pia ametoa wito kwa wakazi wa kijiji
hicho kuchukua tahadhari wakati wakiwa wakitembea popote kwani hiki ni
kipindi cha mavuno ya ngano na kupanda viazi mashambani hivyo kuwa
katika makundi kwani kuna dalili za kuwepo kwa mnyama huyo mazingira
hayo
Post a Comment