WANANCHI WA VIJIJI VYA KATA YA UKWAMA WILAYANI MAKETE WAAMUA KUUNDA BARABARA YAO

Wednesday, November 20, 20130 comments

Wananchi wa Vijiji vya Utweve, Masisiwe na Usagatikwa kata ya Ukwama wilayani Makete wanaendelea na ujenzi wa kuunganisha barabara kati ya vijiji hivyo ulioanza mwaka 2011

Akizungumza na Mtandao huu Mwenyekiti wa kijiji hicho Bw.Lauten Enock Sanga amesema kuwa shirika la TASAPH ndilo lililowataka wananchi wa vijiji hivyo kuibua mradi wowote na wananchi hao wakaamua kutengeneza barabara itakayo viunganisha vijiji hivyo

Amesema mradi huo gharama zote ni nguvu za shirika hilo ambapo walianza ujenzi wa barabara hiyo mwaka 2011 ikiwa hadi sasa mkakati wa ukamilishaji wa kuweka makalavati katika barabara hiyo unaendelea

Hata hivyo amelishukuru shirika la TASAPH kwa jitihada hizo kwani itasaidia hata kukuza kiwango cha uuzaji wa mazao na kurahisisha usafiri kati ya vijiji jirani hivyo na kuongeza kuwa wananchi wameupokea kwa mikono miwili mradi huo ambapo pia umetoa ajira kwa wakazi wa vijiji hivyo kwa kufanya kazi za kukwetua, kufyeka nyasi pamoja na kuchimba barabara hiyo.

Na Furahisha Nundu
Share this article :

Post a Comment

 

Copyright © 2013. MAKETE BLOG - All Rights Reserved
Designed by Edwin Moshi
Property of Makete District Council