Katibu
mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akizungumza na wananchi waliofika
kushuhudia akikabidhi trekta la kulimia alilolikabidhi kwa vijana wa
kata ya kigala tarafa ya ikuwo wilayani Makete hii leo
Katibu
mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahmana Kinana akilima kwa kutumia trekta katika
shamba lililopo kata ya Kigala tarafa ya Ikuwo wilayani Makete
Katibu
mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akikabidhi funguo za trekta kwa
mojawapo wa kijana wa kata ya Kigala wilayani Makete
Mbunge wa jimbo la Makete ambaye pia ni naibu waziri wa maji Dkt. Binilith Mahenge akizungumza katika mkutano huo wa CCM
======
Chama
cha Mapinduzi (CCM) kimesema kitaendelea kufanya kazi na vijana wote
bila kujali itikadi ya vyama vya siasa walivyonavyo kwa kuwa chama hicho
kilipoomba ridhaa ya kuongoza nchi kiliahidi kuboresha maisha kwa
watanzania wote
Kauli
hiyo imetolewa na katibu mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana wakati
akikabidhi trekta kwa vijana wa kijiji cha Mlengu kata ya Kigala
wilayani Makete hii leo
Ndugu
Kinana amesema trekta hilo limetolewa na chama cha mapinduzi ikiwa ni
utekelezaji wa ilani ya CCM ya kuhakikisha wanaiboresha sekta ya kilimo
hasa kwa vijana wakiwemo vijana wa Makete
Amewataka
vijana hao kuendelea kuongeza zaidi kasi ya kilimo kwani ni njia
mojawapo ya kujikwamua kiuchumi, huku akiwasisistiza kulitunza trekta
hilo ili liweze kudumu
Vijana
hao zaidi ya 200 wa kata ya Kigala tarafa ya Ikuwo wameandaa shamba la
zaidi ya hekari 300 ambapo kupatiwa trekta hilo lenye jembe na haro
litasaidia kuinua shughuli za kilimo kwa vijana hao
Wakati
huo huo mbunge wa jimbo la Makete ambaye pia ni naibu waziri wa maji
Dkt. Binilith Mahenge ameahidi kuwanunulia vijana hao tela la trekta
hilo kwa kuwa linahitajika hasa kwa kubebea mazao yao na vitu vingine
mashambani
Ameyasema
hayo wakati akielezea shughuli zinazofanywa na serikali kutekeleza
ilani ya CCM katika mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye viwanja vya
ofisi ya CCM kijiji cha Mlengu
Ndugu Kinana ameambatana na katibu wa NEC itikadi na uenezi Nape
Nnauye, katibu wa NEC siasa na uhusiano wa kimataifa na mbunge mteule
Dkt. Asharose Migiro, viongozi mbalimbali wa chama na serikali wa mkoa
wa Njombe na wilaya ya Makete
Na Edwin Moshi
Post a Comment