Mahakama
ya wilaya ya Makete imemuachia huru Bi.Agness Tweve mkazi wa kijiji cha Iwawa
kata ya Iwawa wilayani Makete Mkoani Njombe aliyekuwa anatuhumiwa kwa kosa la
kumjeruhi Donad Daud Sanga mkazi wa Iwawa Wilayani hapa.
Akitoa uamuzi wa kumuachia huru bila masharti Hakimu wa Mahakama ya wilaya ya Makete
Mh.John Kapokolo amesema kuwa Mahakama imemuachia huru mtuhumiwa kutokana na
ushahidi uliotolewa kutokuwa na vielelezo vya kuaminika mahakamani kuwa
mtuhumiwa huyo alitenda kosa hilo.
Hata
hivyo ushahidi uliotolewa haukuwa wa wazi na kubainisha namna gani mjeruhiwa
ajeruhiwa na kuathirika kwa kiasi gani kwani inaonyesha mshitakiwa alipatwa na
hali mbaya
Wakati
huo huo ndugu Manenge Sanga mwenye umri wa miaka 40 mkazi wa Ilevelo kata ya
Lupalilo wilayani Makete amefikishwa mahakamani hapo kwa tuhuma za kumbaka mwanamke mmoja (jina
limehifadhiwa) mwenye umri wa miaka 65 mkazi wa kijiji cha Ilevelo.
Akisoma
mashtaka hayo mwendesha mashtaka wa jeshi la Polisi Wilayani Makete
Bw.Gozbet Komba amesema mtuhumiwa alitenda kosa hilo mnamo tarehe 7
Julai 2013
saa mbili usiku katika kijiji cha Ilevelo ambapo alimvamia mshtaki akiwa
nyumbani kwake na kumbaka mama huyo
ambaye pia ni Mjane.
Hata
hivyo mshitakiwa amekana kuhusika na mashitaka, ikiwa mwendesha mashitaka wa
polisi Bw.Komba ameiomba Mahakama kuwaleta mashahidi wa shitaka hilo katika tarehe
iliyopangwa ambayo ni tarehe 20 Desemba mwaka huu.
Na Henrick Idawa
Post a Comment