Katibu mkuu CCM Ndg Kinana akizungumza shuleni hapo
Mkuu wa wilaya ya Makete Mh. Josephine Matiro akitoaa taarifa ya shule hiyo kwa katibu mkuu wa CCM na Ujumbe wake
Saruji kwa ajili ya ujenzi ikiteremshwa kwenye lori
Madarasa yakisubiri wanafunzi
Viongozi
wa wilaya wakiongozwa na mkuu wa wilaya ya Makete Josephine Matiro( wa
pili kushoto) wakiangalia mafundi wakichimba msingi wa bweni.
====
Juhudi
zinazofanywa na mkuu wa wilaya ya Makete Mh. Josephine Matiro
kurahisisha upatikanaji wa elimu wilayani mwake zinazidi kung'ara baada
ya neema kuishukia shule ya sekondari ya wasichana iliyopo kijiji cha
Utweve kata ya Ukwama na kuacha raha kwa wananchi walioshuhudia neema
hiyo
Hiyo
ni kufuatia viongozi wakuu wa chama cha mapinduzi (CCM) taifa
wakiongozwa na katibu wao Ndugu Abdulrahman Kinana kutembelea shule hiyo
ambayo bado inaendelea kujengwa na kuahidi mbele ya hadhara
iliyohuduria kuwa CCM Taifa itatoa mabati 200 kwa ajili ya ujenzi katika
shule hiyo
Katibu
mkuu Ndg Kinana ndiye aliyetoa ahadi hiyo mara baada ya kujionea nguvu
za wananchi, mfuko wa maeendeleo ya jamii TASAF na halmashauri ya wilaya
ya Makete kuunganisha nguvu zao na kufanikiwa kujenga vyumba vitatu vya
madarasa, nyumba ya mwalimu pamoja na vyoo
Awali
akitoa maelezo mafupi kuhusu shule hiyo, mkuu wa wilaya ya Makete Mh.
Josephine Matiro amesema shule hiyo ni ya kwanza wilayani hapo kuwa na
wanafunzi wasichana pekee, hivyo wanatarajia kuanza kupokea wanafunzi
Januari mwakani
Amesema
kwa sasa wanajenga hosteli kwa ajili ya wanafunzi hao, ila kwa kuanzia
watatumia chumba kimoja cha darasa kama hosteli wakati ujenzi wa bweni
ukiendelea, huku akiomba kusaidiwa bati 200 kwa ajili ya shule hiyo,
ambazo zitatolewa na CCM kwa ahadi ya katibu mkuu wa CCM
Mtandao
huu umeshuhudia vifaa vya ujenzi vikishushwa shuleni hapo ikiwemo
mifuko 100 ya saruji, na mafundi wakiendelea kuchimba msingi wa mabweni
hayo
Matiro
amesema ujenzi wa shule hiyo ni utekelezaji wa ilani ya CCM yenye
kutaka kuhakikisha elimu inawafikia wanafunzi wote wanaotakiwa kuipata
bila kujali itikadi ya kitu chochote, na kuongeza kuwa ushirikiano
alioupata kutoka kwa wakazi wa makete ambao wanakaa nje ya wilaya hiyo,
kwani nao wanashiriki kwa pamoja na serikali na wadau wote kuhakikisha
shule hiyo inakamilika
Habari/picha na Edwin Moshi
Post a Comment