Umoja wa wanawake wa chama
cha mapinduzi kata ya Isapulano wamekabidhiwa mradi wa nguruwe wenye thamani ya shilingi
laki mbili na themanini na Mh.diwani wa kata ya Isapulano Aginiwe Mahenge kwa niaba ya Mbunge wa Jimbo la Makete
Akikabidhi nguruwe hao kwa
niaba ya mbunge Binilith Mahenge ambaye ni mbunge wa jimbo la Makete, diwani huyo amewataka wana kikundi hicho kutunza nguruwe hao ili
kuendelea kuongeza kipato ili waweze kujikwamua kwenye wimbi la umasikini.
Kwa upande wake mwakilishi wa
kikundi hicho Bi. Etelinah Mahenge amemshukuru Mh. mbunge kwa kutoa msaada huo na
kuahidi kuwa watautunza mradi huo kwa hali na mali ili kuongeza kipato katika maisha yao.
Nguruwe hao wametolewa na mh.
mbunge wa Makete ikiwa ni ahadi yake aliyoitoa tarehe kumi na tano septemba
mwaka huu wakati wa ziara yake kijiji hapo.
Na Riziki Manfred
Post a Comment