Kazi
ya kusambaza kifusi sekunde chache baada ya kumwagwa na lori barabarani
ikiendelea kama ilivyonaswa na mwandishi wetu eneo la Mago wilayani
Makete.
Wananchi
wilayani Makete mkoani Njombe wamempongeza mkandarasi anayekarabati
barabara kuu Makete - Njombe katika kata ya Lupalilo kutokana na
kitendo cha kulundika vifusi na kuvisambaza papo hapo
Inadaiwa
kuwa mkandarasi huyo kuwenda akawa wa kwanza kufanya kitendo hicho
wilayani hapa kwani wengi wamekuwa wakivilundika vifusi barabarani na
kuviacha muda mrefu bila kuvisambaza hali inayosababisha kwero kwa
watumiaji wa barabara hiyo
Mtandao
huu umeshuhudia lori moja linapomwaga kifusi, greda linakisambaza
kwanza na ndipo lori lingine linatakiwa kumwaga kifusi kingine
Hali
hiyo imeonesha kuwafurahisha wengi hasa watumiaji wa barabara hiyo kwa
kuwa hakuna usumbufu wa mlundikano wa vifusi kwa muda mrefu kama
ilivyozoeleka kwenye suala zima la ujenzi wa barabara
barabara
hiyo iliyopo chini ya TANRODS Njombe inaendelea na matengenezo ambapo
kwa sasa wapo katika kata ya Lupalilo kuendelea na ujenzi huo
Na Edwin Moshi
Post a Comment